Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Stephen Wasira amewatahadharisha wanachama wa chama hicho wenye dhamira kugombea nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi mku unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba kujiepusha na Kampeni za mapema kwani ni uvunjifu wa maadili.
“Kazi yangu ni kusimamia maadili hasa watu wanaotaka ubunge wameanza kunyemelea na wananyemelea kuvunja maadili tunawata mpige kura mkiwa watu huru na muiambie CCM tukimsimaisha huyu tunashinda bila tabu kama atakayeshinda akiwepo samia na hapa tunataka mmoja tu”
Wasira amesema kuwa ana habari na wanaotaka kugombea ubunge kuwa wameanza kuvuruga maadili “Wale wanaotaka ubunge nina habari zao nina habari zao wameanza kuvuruga maadili wanataka muwapigie kura kwa hela wanazowapa”
Aidha Makamu Mwenyekiti huyo amewataka wagombea wote wapya na waliopo kuacha kusamba hela kwa wajumbe ili wawapigie kura kwani kazi ya ubunge sio kusambaza hela bali ni kusambaza huduma katika jamii.
“Na hili nalisema kwa wagombea wapya na kwa wabunge waliopo tunachunguza tunajua mwenendo huu kuna mahali pengine wanazidisha kabisa mambo mpaka yanatia kinyaa hasa naawambia achaneni na hiyo wacheni kupofusha wajumbe”
.
.
.#tanzania #eastafrica #bagamoyo #citizen #ccm2025 #ccm #samia #fyp #politics #instagram #tiktokviral #tanzania #mustleadtv #zanzibar
