Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amethitisha taarifa za msemaji wa klabu ya Yanga Ali Kamwe kukamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kufuatia matamshi yake kwa viongozi wa serikali wakati timu ya Yanga ikijiandaa na mchezo wake na Timu ya Tabora United.
