Wizara ya TAMISEMI imetoa fursa ya mwezi mmoja kwa Wanafunzi waliohitimu Kidato cha Nne mwaka 2024 kubadili tahasusi zao (combination) au Kozi kwa wale watakaopangiwa vyuo vya serikali ambapo utaratibu huo umeanza tangu Machi 31 na mwisho unatarajiwa kuwa ni Aprili 30 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema ““Hatua hii ni maandalizi ya awali ya uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga Kidato cha Tano na Vyuo vya Serikali kwa mwaka 2025.”
Serikali imekuwa ikitoa fursa kwa wahitimu wa Kidato cha Nne kufanya mabadiliko ya machaguo ya Tahasusi (combination) na Kozi mbalimbali walizozichagua kupitia Fomu ya Uchaguzi (Selform.).
Fursa hii huwawezesha wanafunzi kurekebisha machaguo yao kulingana na ufaulu waliopata kwenye matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).

Mchengerwa alisema Serikali kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI imekamilisha utaratibu wa awali wa kuingiza kwenye kanzidata taarifa zilizo kwenye fomu za uchaguzi za wanafunzi kama zilivyojazwa na wanafunzi wakiwa shuleni.

“Baada ya wanafunzi kufanya marekebisho yao, kanzidata hiyo ndiyo itakayotumika kuwachagua na kuwapangia nafasi za Kidato cha Tano na Kozi mbalimbali katika Vyuo vya Kati na vya Elimu ya Ufundi kwa kuzingatia sifa za ufaulu na machaguo yao.”
.
.
. #tamisemi #mustleadtv #elimu #fypツ #fypviral #instagramreels #tanzania #facebookreels

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *