Kuelekea mcheza wa marudiano wa hatua ya robo fainali ya kombe la Shirikisho Afrika, kati ya timu ya Simba SC na Al Masry, msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Ally amesema mgeni maalum kwenye mchezo huo atakuwa ni Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Walace Karia.
Msemaji huyo wa Simba amesema kuwa “Walace Karia ametenda mema mengi sana kwa mpira wa Tanzania na mafanikio tuliyokuwa nayo simba katika anga za kimataifa ni kutokana na uimara na ubora wake Wallace Karia”
Timu ya Simba inajiandaa na mchezo huo utakaochezwa siku ya Jumatano Aprili 09 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ikiwa kumbukumbu ya kupoteza kwa kufugwa mabao 2-0 ugenini.
.
.
.
#simba #yanga #dar-es-salaam #tanzania #cafccl #ahmedally #allykamwe #mustleadtv #habari #michezo #eastafrica #fyp #viral #facebook #instagramreels #tiktokkenya #tiktoktz
