UTAJIFUNZA NINI Utakapomaliza kukisoma kitabu hiki, utapata maarifa ya namna ya kuwa mtunzi wa vitabu kwenye fani yako. Utajua namna ya kutambua mada ndogo ndogo kwa urahisi ili uandike kitabu chako. Utafahamu namna ya kupata muda wa kuandika kitabu na kukadiria masaa na siku unazohitaji kukamilisha kitabu chako, tena ndani ya ratiba yako yenye mambo mengi bila kuathiri kazi zako nyingine. Utafahamu nini maana ya ISBN na namna ya kuipata na umuhimu wake kwenye kitabu chako. Utapata mwanga wa sehemu unayoweza kwenda kuchapa kitabu chako kwa haraka na gharama nafuu. Utapata maarifa ya soko na mauzo ya vitabu hususani kwa uzoefu wa Tanzania. Mwisho, nimekuwekea mambo 12 muhimu yatakayofanya kitabu chako kiwe na mvuto kwa wasomaji wako. Nakualika endelea kusoma sasa kitabu hiki kwa amani. Peter Mkufya Mkufunzi na Mhamisishaji Maendeleo Kweli Program Whatsaap +255 786 202 202
KITABU CHA MAARIFA YA FEDHA
KWANINI USOME KITABU HIKI Binadamu wote tunahitaji kujua maarifa ya fedha. Nafahamu kabla ya kugunduliwa fedha, maarifa haya hayakuwa muhimu kama leo. Kipindi hicho, jambo muhimu ilikuwa ni uzalishaji. Unavyozalisha bidhaa nyingi zenye dhamani unakuwa na uwezo mkubwa wa kubadilishana bidhaa mbali mbali na watu wengine. Mfumo huu uliitwa Bata Tredi (Barter trade system). Maarifa ya fedha na namna ya kuzikamata kwa karne hii hayaepukiki kwa sababu nyingi. Mwenye maarifa haya anauwezo mkubwa wa kujua namna ya kutengeneza fedha zaidi, kujua namna ya kuzihimili gharama na kuziepuka pale inapostahili, anajua mikopo salama na namna ya kuangalia vigezo vya ukopaji, anajua kuweka kumbukumbu zake vizuri, anafahamu kuandaa bajeti yake n.k. Kupata maarifa ya mambo haya, kunasaidia watu kutatua changamoto mbalimbali za kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiroho na kiutamaduni. Nimekaa karibu na wavuvi nakujifunza mengi. Nimefika kipindi nikaona kukamata Samaki ni kama kutafuta fedha. Fedha ni kama Samaki. Fedha inateleza kama samaki, pia fedha inayeyuka kama barafu. Hizi ni baadhi ya tabia za fedha.


