Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) Dkt. Charles Kichere amesema kuwa deni la serikali limeongezeka hadi Trilioni 97.35 kutoka Trilioni 82.25 mwaka 2022/23. Dkt Kichere amesema hayo leo ikulu jijini dar es salaam wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea taarifa ya mwaka ya utendaji kazi wa TAKUKURU na ripoti ya CAG kwa mwaka 2023/24.
“Kufikia tarehe 30 June Mwaka 2024 deni la serikali lilifikia shilingi trilioni 97.35 kiasi hiki kimeongezeka kutoka trilioni 82.25 kilichokuwa kimeripotiwa mwaka 2022/23 hii ni sawa na ongezeko la shilingi trilioni 15.1 ambalo ni sawa na asilimia 18.36 deni hilo linajumuisha deni la ndani la trilioni 31.95 na deni la nje la trilioni 64.40.
Mkaguzi mkuu wa serikali ameongeza kuwa deni la Serikali bado ni himilivu ” Mheshimiwa Rais tathmini deni la Serikali imebaini kuwa deni la taifa bado ni himilivu viashiria vikuu vinaonesha kuwa thamani halisi ya deni la nje ni asilimia 23.6 ya pato la taifa chini ya ukomo wa asilimia 40 na deni la jumla ni asilimia 41.1 ya pato la taifa chini ya ukomo wa asilimia 55

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *