Utambuzi wa maono yako – Moto ndani yako

Maono aliyokupa Mungu yatekeleze haraka. Yeye ndio mtendaji. Wewe ni mfanyakazi katika Shamba lake.

Mfanyakazi katika shamba kazi yake kubwa nikutimiza wajibu na maelekezo akiyopewa, nikusimamia ufanisi wa utekelezaji wa kazi za wengine shambani ili malengo yafikiwe.

Kuhusu pembejeo na rasilimali nyingine ni kazi ya mwenye shamba. Jambo la msingi nikumpa taarifa.

Kwa maana hiyo maono uliyopokea Toka kwa Mwenyezi Mungu, pamoja na ukubwa au udogo wake, Anza yatekeleze.

Mifano aliyotupa Bwana Yesu, inaonyesha wazi, tumeachiwa wajibu wa kufanya katika dunia hii. Tutatakiwa kutoa hesabu.

Nyumba ninayoishi huko shambani kwangu, waliingia nyuki juu ya dari. Wamekaa huko kwa miezi mingi.

Siku Moja asubuhi nyuki mmoja akatoka, akazunguka chumbani, nikapata wasiwasi pengine asije kunigonga. Baada ya muda akatua chini na kutembea. Akaingia sehemu ambapo maji yalimwagika. Nimaji kidogo sana. Akaanza kupata tabu. Akabinuka binuka. Mbawa zake zikalowa. Akalala hapo, akafa. Maji yalikuwa kidogo sana sakafuni lakini nyuki alipata shida kutoka, akakwama asiweze kufanya kitu tena.

Tukio hili likanizamisha juu ya maono. Kazi ufanyayo ikiwa ni yakimaono itafanikiwa. Ikiwa si yako mazingira yatakuwa si wezeshi kwako. Utapanda havikui. Vikikua havizai. Vikizaa hakuna Soko. Hii inatusisitimiza umuhimu wa matumizi ya kanuni yetu ya K.W.E.L.I kuwa tuanze na Imani (Imani) badala ya kuanza
na Kipato (K).

Dunia inapotea na wengi wanapotea kwa kuanza kutafuta Kipato (K), wanatumia vibaya kanuni ya KWELI, badala ya kutoka kushoto kwenda kulia, wanatoka kulia kwenda kushoto mwa kanuni ya KWELI. Maisha yanazidi kuwa magumu. Unakosa ubunifu. Una kopi na kupesti – unaiga maono na ndoto za watu.

UNAPOANZA na Imani nikusema unajitafuta kwanza. Unaangalia karama na maono atakayokupa mwenyezi Mungu ili kazi yako, isikwame, isife kama yule nyuki. Fuatilia mafunzo ya kanuni ya KWELI kwa Mafanikio yako kimaono.

Angalia sana ule mradi unaowaka moto ndani ya moyo wako mara kwa mara na kwa muda mrefu. Ufanyie kazi. Hii ni njia ya kujua maono yako na kujua Mwenyezi Mungu anataka ufanye nini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *