KWANINI NAHIMIZA MIRADI

KWANINI NAHIMIZA MIRADI

HIVI karibuni niliandika tofauti kati ya Mradi na Biashara.

JAPO biashara huongeza kipato na kukuza uchumi, faida za kufanya mradi ni nyingi.

NILIFUNDISHA namna ya kugeuza biashara kuwa mradi, ili uone faida zaidi kiuchumi na kijamii (audio ipo, wasiliana nami)

LEO napenda ufahamu kuwa, mradi unao upenda unaweza kuuvunja-vunja, yaani kuuweka katika sehemu ndogo ndogo ili kurahisisha uanzishwaji wake.

JAPO andiko la mradi linabeba taarifa za mradi kwa mapana yake, unaweza kuanza mradi wako kidogo kidogo (Ipo Audio ya Jinsi ya Kuandika Andiko la Mradi, tuwasiliane)

PICHA pana ya mradi wako ni muhimu, lakini usikuvuruge. Isikuletee hofu ya kuanza.

MOJA ya mkakati muhimu unaotakiwa kuwa nao, ni kuanza. Anza na chochote maadam kina mchango wa maana kwenye mpango mkubwa wa mradi wako (The master plan)

NAFURAHISHWA na miradi kwa sababu inabeba ndoto, wito na karama za watu. Ni moja ya njia ya kuacha alama isiyofutika kwenye jamii.

MRADI mzuri, unagusa maisha na uhai wa watu. Naendelea kukuhamasisha, uanzishe mradi na kama unayo tayari, basi ongeza UFANISI, UGUNDUZI na UVUMBUZI.

@drpetermkufya

#mustlead
#moyompya
#kweli

Follow me for more….https://chat.whatsapp.com/GJYDw4XzqLIF7LjBiIHJxb

www.petermkufya.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *