Sale!

Ufugaji wa kuku kibiashara

Sh5,000

Kuku ni jamii ya ndege alietokana na jamii ya kuku-mwitu mwekundu wa huko Asia. Baada
ya muda fulani kupita mwanadamu alitambua kuwa kuku anaweza kufugika kirahisi. Hata
hivyo, ufugaji rasmi kwaajili ya biashara ulianza katika karne ya kumi na tisa (19) na leo
nyama ya kuku inatumika zaidi kuliko nyama ya ndege mwingine yeyote. Mamilioni ya watu
walioko katika jamii ya makundi mbalimbali ya wale wanaoishi vijijini na mijini hufuga kuku
kwa ajili ya chakula na biashara.


Inakadiriwa kuwa kuna aina za kuku asilia wapatao hamsini na sita (56) hapa nchini ambao
wanachangia asilimia thelasini (30%) ya pato la jumla (GDP) litokanalo na mifugo (5.9%).
Huu ni ushahidi tosha kuwa iwapo kuku wa asili watafugwa na kuhudumiwa kwa misingi
imara pato litaongezeka maradufu na kuleta tija kwa familia na kwa wafanyabiashara wengi.
Katika karne ya ishirini na moja (21), kuku wanafugwa na kuzalishwa kwa sababu mbalimbali
na kuna vyombo husika vinavyo simamia viwango vya usanifu (standards) wa uzao wa aina
ya kuku wanaotakiwa kuzalisha hapa nchini. Vyombo vya kwanza kuchunguza ni kama vile
The British Poultry Standards, The Australian Poultry Standards na American Bantam
Association ambao wao huhusika na kuku wadogo (Vifaranga

Scroll to Top