Sale!

Kilimo cha papai kibiashara (Copy)

Sh4,500

Category: Tag:

Papai ni moja ya tunda mashuhuri linalo LIMWA NA KUTUMIKA kwa kiasi
kikubwa nchini Tanzania. Inasadikika asili ya Papai ni maeneo ya Tropiki huko
Amerika, kusini mwa Mexico na nchi kadhaa za Amerika ya Kati. Tunda hili
lina faida mbalimbali za afya kwani lina Sukari, Vitamin A na C na katika
kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili. Utomvu wa Papai bichi hutumika
kulainishia nyama na kutengeneza dawa mbalimbali. Kilimo cha zao la Papai
kinaweza kuwa chanzo kikubwa cha pesa za kigeni kama zao hilo likiuzwa
nje ya nchi. Uzalishaji wa Papai nchini Tanzania ni wa kiasi Kidogo (Trakribani
Tani 2,582) kwa Mwaka kulinganisha na watumiaji wa zao hilo. Hivyo, hii ni
fursa mwanana. Inahitajika watu wengi zaidi kuwekeza katika uzalishaji wa
Papai. Papai ni tunda linalochukua muda mfupi hadi kufikia mavuno.
Huchukua muda wa miezi 8 hadi 9 kufikia mavuno. Pia wataalamu
wanasema mavuno makubwa huweza kupatikana kuanzia mwaka wa pili
wa mavuno na kuendelea. Papai ni fursa nzuri. Rais Mstaafu wa Awamu ya
Nne Tanzania, Dr. Jakaya M. Kikwete naye amehamasika na fursa ya Kilimo
cha Papai (Adamu Nyamagange, 2018).

Scroll to Top