Mkufunzi miradi, ujasiriamali, kilimo biashara na maendeleo.

Dr Peter Mkufya (PhD) Peter Mkufya (PhD) niĀ  Mkufunzi wa masuala ya Fedha, Mwandishi nguli wa vitabu, Mwandishi wa mapendekezo ya miradi na Mwanzilishi wa kampuni na shule za MustLead. Amechukua umaarufu mkubwa kwa kuandika vitabu mbalimbali kama Moyo Mpya, Maarifa ya kupata mtaji fedha, Ujasiriamali na Mbinu za Kujiajiri, Maarifa Ya Fedha, Tetemerko la Ujana, Kijana mwenye ndoto kubwa, Moyo Mpya, Mbinu za kuongeza mauzo, Why you should not lose hope, Matukio yanazungumza na vingine vingi. Amefanya kazi katika Sekta ya Kilimo kwa zaidi ya miaka kumi na minne baada ya kuhitimu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA). Baadhi ya kampuni na mashirika aliyoyafanyia kazi ni Kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco kama Meneja Mradi na Utawala mwaka 2004 na kuwa Mfanyakazi Bora wa Taifa mwaka 2006. Ana Shahada ya Sayansi ya Kilimo (Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine 2004), Shahada ya Uzamili katika Maendeleo Vijijini (Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine 2010) na shahada ya Udaktari wa Falsafa katika Maendeleo ya Uchumi wa Jamii (PhD in community economic development)

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top